Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya tamko la Hawza za Mabanati katika kulaani jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni nchini Yemen ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
"Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu, Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao."
(Surat Ibrahim, Aya ya 42)
Hawza za Mabanati, kwa sauti yenye uwazi na mioyo iliyojaa huzuni na ghadhabu, zinalaani vikali shambulizi la kigaidi na kijinai la hivi karibuni lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya baraza la mawaziri nchini Yemen na kuuawa kishahidi kwa dhulma Waziri Mkuu na kundi la mawaziri.
Viongozi wa Yemeni walilengwa kwa kosa pekee la kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina na kulinda haki yao ya kihistoria na halali dhidi ya uvamizi, kitendo hiki cha kinyama kwa mara nyingine kimeonesha uso wa kigaidi na kinyama wa utawala wa Kizayuni, na kudhihirisha kwamba kundi hili la jinai, kwa msaada wa Marekani, baadhi ya nchi za Ulaya na baadhi ya tawala za Kiarabu, halitii misingi ya kibinadamu na kanuni za kimataifa.
Kimya kizito na kutochukua hatua kwa mashirika ya kimataifa na tawala za Kiarabu za ukanda huu mbele ya janga hili ni sawa na kuwasha taa ya kijani kwa kuendelezwa mauaji ya kimbari na ukatili dhidi ya mataifa madhulumu.
Iwapo mashirika haya na tawala hizi za Kiarabu zingelikuwa na utiifu hata kidogo kwa wajibu wanaodai, walipaswa kusimama kinyume na dhulma na umwagaji damu huu tangu miaka iliyopita.
Lakini ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya hakika na thabiti kwamba mwisho wa jinai hizi zisizo na mfano utakuwa ni maangamizi na kuporomoka kwa utawala wa Kizayuni na fedheha ya waungaji mkono wake, historia inashuhudia kwamba dhulma haidumu, na moto ulio washwa leo Yemen na Palestina, pia utayateketeza mataifa hayo ya Kiarabu na ya Magharibi.
Wanafunzi, walimu na wafanyakazi wa Hawza za Mabanati nchini, pamoja na kuonyesha rambirambi zao kwa taifa thabiti la Yemen na familia tukufu za mashahidi, wanasisitiza tena kwamba njia pekee ya kukabiliana na utawala haramu wa Israel, ambaye ni mfano dhahiri wa shari tupu, ni kuendeleza mapambano na mshikamano kwa umma wa Kiislamu, na ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu nusra ya upande wa haki iko karibu na ni ya hakika.
" Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka."
Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Mabanati
Maoni yako